Real Madrid kuchuana na Atalanta kwenye ngarambe za UEFA Super Cup

Aug 14, 2024 - 20:33
 0
Real Madrid kuchuana na Atalanta kwenye ngarambe za UEFA Super Cup
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Real Madrid watachuana na Atalanta kwenye ngarambe za UEFA Super Cup mnamo Jumatano usiku.

Real Madrid wanatarajia kutoana kijasho na Atalanta saa nne usiku saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Kitaifa wa Warszawa katika taifa la Poland. 

Kikosi cha Real Madrid kitakachoanza mechi ya leo ni Thibaut Courtois, Dani Carvajal, Eder Millitao, Antonio Rudiger, Ferland Mendy, Federico Valverde, Aurelien Tchouameni, Luca Modric, Jude Bellingham, Kylian Mbappe na Vinicius Junior.

Kwa upande wa timu ya Atalanta kuna Juan Musio, Berat Djimsiti, Isak Hie, Sead Kolasinac, Davide Zappacosta, Ederson, Marten De Roon, Matteo Ruggeri, Charles De Ketelaere, Mateo Petegui na Ademila Lookman. 

Los Blancos wanatumia mfumo wa 4-3-3 ilhali Atalanta wanatumia mfumo wa 3-4-3.

Ujio wa Kylian Mbappe katika timu ya Real Madrid utaongeza makali katika Kikosi cha Real Madrid chake Carlo Ancelotti. 

Kuna uwezekano mkubwa wa Real Madrid kuibuka mshindi kwa sababu Kylian Mbappe amejumuishwa katika kikosi cha Kwanza cha mchuano wa leo.

Kylian Mbappe kwa ushirikiano na Vinicius Junior na Jude Bellingham watawezesha Los Blancos kupenyeza upesi kwenye safu ya ulinzi ya Atalanta. 

Kufikia sasa Real Madrid wameshinda UEFA Super Cup mara tano. 

Mara ya Kwanza walishinda mwaka wa 2002, 2014, 2016, 2017 na 2022 mtawalia huku wakicheza fainali mara tatu.

Mabingwa hao wa uhispania wamecheza katika mashindano 26 bila ya kushindwa.

Mahasidi wa Real Madrid Atletico Madrid waliwafunga mabao 4-2 katika dakika za nyongeza katika michuano ya Copa del Rey mnamo January, 2024.

Hii ni mara ya tatu kwa timu ya Real Madrid na Atalanta kukutana kwa mashindano haya. 

Real Madrid walitawazwa washindi wa Laliga kwa mara ya 36 huku Atalanta ikimaliza ya nne katika Ligi ya Serie A msimu uliopita. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow