Viongozi Mlima Kenya waonywa kusitisha siasa za chuki
Na Robert Mutasi
Viongozi wa kisiasa na wachanganuzi wa siasa kutoka eneo la Mlima Kenya wametoa onyo kali kwa viongozi eneo hilo kuasi siasa za chuki na badala yake kufanyia Wakenya maendeleo.
Viongozi hao walieleza kuwa siasa hizo za chuki huenda zikatatanisha ukuaji wa maendeleo nchini.
Waliwakosoa vikali viongozi wanaeneza semi za kusambaratisha amani katika eneo hilo.
Baadhi ya viongozi kutoka Mlima Kenya wamekuwa wakieneza uvumi wa hoja za kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani.
Hii inafuatia msimamo wake Gachagua wa kuunga mkono mfumo wa ugawaji fedha za serikali kwa kuzingatia idadi ya watu.
Hatua hiyo ya Gachagua ilionekana kuleta upinzani mkali miongoni mwa viongozi eneo hilo.
Wachanganuzi wa siasa pamoja na viongozi kutoka Mlima Kenya wameendelea kuwapinga vikali viongozi kutoka eneo hilo wenye njama ya kuleta mapinduzi katika serikali huku wakiwa taka kukoma kumpiga vita Gachagua.
Walihoji kuwa ni vyema kwa viongozi hao kuzingatia kuwahudumia Wakenya na kufanya kazi kwa ukaribu na Naibu Rias kwa manufaa ya taifa.
Naibu Rais alionekana kukerwa na hatua ya baadhi ya viongozi kutoka Mlima Kenya kuhusu kubanduliwa kwake na kuwaonya kutoeneza semi zitakazogawanya Wakenya.
Aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria ni miongoni mwa viongozi waliojitokeza wazi na kumtetea Naibu Rais Gachagua huku akimuunga mkono kwa msimamo wake.
Baadhi ya wa bunge kutoka eneo la Mlima Kenya waliimsihi Gachagua kuacha kujipigia debe siasa za 2027 na badala yake kuhudumia Wakenya kwanza.
Kumekuwepo na madai kutoka kwa wachanganuzi wa kisiasa na vyombo vya habari kuhusu uhusiano baina ya Rais William Ruto na Rigathi Gachagua kwamba umeyumba.
Lakini Gachagua amekuwa akiyapinga madai hayo ya kutokwa na uhusiano mzuri na Rais Ruto akisema kuwa uhusiano wao ungali imara.
Gachagua aliwakosoa baadhi ya viongozi wanaompiga vita kutoka Mlima Kenya kumheshimu kama naibu rais.
What's Your Reaction?