Polisi wanasa bangi yenye thamani milioni mbili

Aug 1, 2024 - 20:06
Aug 1, 2024 - 21:36
 0
Polisi wanasa bangi yenye thamani milioni mbili
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Maafisa wa polisi wamenasa bangi yenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni mbili, katika mtaa wa Kayole, Naivasha.

Kulingana na Naibu Kamishna Kaunti ya Nakuru, Josiah Odongo,bangi hiyo ilikuwa inakadiria uzito wa mizani ya kilo 70.

Akizungumza na waandishi wa habari mnamo Alhamisi, Agosti 1, 2024, Odongo alisema kuwa bangi hiyo ilipatikana katika chumba cha kukodi katika mtaa wa Kayole, mjini Naivasha.

Odongo alielezea kuwa bangi hiyo ilikuwa imeundwa mfano wa vifagio na nyingine ilikuwa imesagwasagwa.

"Tumeweza kunasa bangi yenye jumla ya kilo 70 inayojumuisha vifagio na pia bangi iliyochakatwa.

"Hii inakadiriwa kuwa Shilingi milioni 2.1 za Kenya," alisema. 

Shughuli hiyo ya msako mkali ilihusisha vitengo tofauti vya polisi ndiposa wakafanikiwa kunasa. 

 Polisi wamedokeza kuwa maeneo hayo ya Naivasha haswa mtaa wa Kayole, yana idadi kubwa ya satu kitu ambach amesema ni vigumu kubaini wahusika wa dawa za kulevya wakati wa kuwasaka. 

Amewapongeza wakazi wa eneo hilo kwa kuwasaidia maafisa wa polisi wenye msako wa kutafuta wahusika wa dawa za kulevya maeneo hayo. 

"Ninataka kuwashukuru wananchi kwa kushirikiana nasi kufanikisha hili na pia ningependa kushukuru timu ya mashirika mengi inayojumuisha Kamati ya Usalama ya Kaunti Ndogo na ACC ya mji wa Naivasha na NGAO kwa juhudi za ushirikiano zilizotuwezesha kunasa. , karibu tukose hii ikiwa hatungekuwa tunafanya kazi kwa karibu," alisema. 

Dawa hiyo ya kulevya inasemekana ilikuwa inasafirishwa kuenda taifa jirani la Tanzania. 

Katika harakati za msako wa dawa hiyo ya kulevya, mhusika mkuu alitoroka lakini polisi wakafanikiwa kunasa bangi hiyo. 

Msako huo uliochukua siku nzima kukamilika, unajiri baada ya wakaslzi kupiga ripoti kwa polisi. 

Kwa mujibu wa polisi, walanguzi wa dawa za kulevya wamekuwa wakiuzia dawa hizo kwa watoto wa shule,kitendo ambacho ni kinyume na sheria. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow