Wazee wa jamii ya Kikuyu waairisha upashwaji tohara mwaka huu

Aug 8, 2024 - 19:53
Aug 8, 2024 - 22:10
 0
Wazee wa jamii ya Kikuyu waairisha upashwaji tohara mwaka huu
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Baraza la wazee kutoka katika jamii ya Kikuyu wameelezea sababu za kuairisha shughuli ya kupasha tohara kwa watoto wa kiume mwaka huu.

Wazee hao amesema kuwa wamesubiri watoto wa kiume wajiunge na shule za upili ndiposa wapashwe tohara.

Kulingana na wazee hao, kutahirisha watoto wakiwa hawajahitimu kiumri hukosa maana kwa kuwa wengi hawajakomaa kiakili. 

Kwa sasa watoto wengi wako katika darasa la nane na gredi ya tisa. 

Wazee hao walisisitiza kuwa endapo wataendesha huduma za tohara mwaka huu haswa kwa watoto ambao bado wangali shule ya msingi, hakutakuwa na mabadiliko yoyote. 

Walisema kuwa mafunzo yanayotolewa jandoni ni ya utu uzima na humuandaa mtoto wa kiume kuwa mtu mzima katika jamii. 

Wanatarajia kufanya shughuli hiyo ya tohara mwaka ujao. 

Wazee hao wa "Kiama Kia Maa" walifafanua kwamba kupashwa tohara kwa watoto waliokomaa huwafaidi sana katika maisha yao kwani huchukua mawaidha wanayopewa na wazee hao wanapotoka jandoni na kuyafanyia kazi katika safari yao ya maisha.

Hata hivyo, wazee hao wamewakashfu wale wanaendesha shughuli ya tohara kama biashara pasi na kuzingatia utaratibu wa jamii hiyo. 

Walitetea shughuli hiyo ya tohara kuwa ndiyo nguzo ya kukuza maadili na ujasiri kwa watoto wa kiume katika siku za usoni. 

Waliwashauri wananchi kutoka jamii hiyo kutokaidi amri yao ya kupasha tohara watoto wao. 

Wazee hao wametaja tohara kama mojawepo ya sherehe muhimu katika jamii hiyo ya Kikuyu. 

Tohara ni daraja la kumtoa mtoto wa kiume kutoka utotoni hadi utu uzima. 

Aidha, wazee hao wamepongeza mtaala wa umilisi kwamba unawapa watoto wao nafasi ya kukua na kujielewa.

Sherehe hizo zilikuwa zinatarajiwa kufanyika , mwezi Agosti, 2024. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow