Uhaba wa maji Tharaka

Nov 13, 2024 - 14:05
Nov 13, 2024 - 14:09
 0
Uhaba wa maji Tharaka
Photo Courtesy.

Tharaka Nithi, 

Wednesday, 13 November, 2024 

By Margaret 

Maji ni neno lenye herufi nne lakini umuhimu wake ni mkubwa mno kwenye maisha kiujumla.

kwa maisha ya kila siku ya shughuli za hapa na pale maji huhitajika kwa asilimia kubwa zaidi hivyo basi kukosekana kwa maji husambaratisha mengi zaidi.

Kutokana na ukame unaoshuhudiwa katika eneo la mlima kenya mashariki hususan katika kaunti ya tharaka nithi. Uhaba wa maji umekuwa kero kuu kwa wakaazi wa eneo hilo la Tharaka ,wanafunzi wa chuo kikuu cha Tharaka wakilaizimika hata kufunga safari ya mbali na mitungi mgongoni,ili kutafuta maji katika vijito vinavyopatikana eneo hilo.

Wanafunzi pia wameelezea kutofanya usafi wa nyumba ,mavazi na hata ukosefu wa maji ya matumizi ya ndani kama vile kuoga,mapishi na hata kunywa ikiwalazimu wengi wao kutohudhuria mafunzo shuleni.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Tharaka Mutemi Junior, Uhaba wa maji ni tatizo la linaathiri hali ya elimu kwa kiwango kikubwa. 

"Nmetoka maeneo ya Nkubu, Kaunti ya Tharaka Nithi ,Uhaba wa maji umekua kero kuu sana katika hili kubwa huku wengi wetu tukilazimika kuchimba mabwawa ya kujikimu ila pia kwa kiasi kikubwa hunyauka kwa sababu ya ukame , Wanafunzi katika Chuo hiki cha Tharaka wamekua wa kusumbuka sana kwa kukosa hata maji ya majukumu ya ndani" Mutemi. 

Ukosefu wa maji eneo hilo umepelekea ukulima kuathtirika kwa kiasi kikubwa mno,kwa kuwa ardhi imenyauka huku rotuba nayo ikikosekana kabisa hivyo basi kupelekea wakulima kutokuwa na imani tena na upanzi katika migunda yao.

lishe katika eneo hilo imezorota kwa kukosa chakula cha kutosha ,na hivyo basi kuongeza bei ya mazao chache inayovunwa na baadhi tu ya wakaazi wanaobahatisha katika misimu ya mvua. 

Njoroge ni mmoja wa wakulima hapa Tharaka Nithi alikuwa na haya ya kusema "Kwanza kabisa ukulima umeathirika sana katika eneo pana hili la Nithi,huku misimu ya kupanda nayo pia ikikosekana kwa kukosa kutabiri msimu wa mvua na kiangazi kwa kuwa ukame umekua wa kushuhudiwa sana upande huu,sisi kama wakulima katika eneo hili tumekosa hata manufaa kwa kuwa hatuleti lishe kwa jamii hivyo basi kusababishia suala kuu la utapiamlo na kuongeza bei ya vyakula vya kimsingi kwa jamii".

Mimea nayo kwa ujumla hata na miti pia ,imekosa maji ya kutosha hivyo basi kunyauka kwa kuwa mizizi haipati maji ya kutosha ili kustahimili ukuaji au uwepo wa miti hiyo. mvua mara mingi hunyesha eneo hilo majira ya Desemba na Aprili ,ila bado haitoshi kuifanya Tharaka kuwa eneo lenye rangi ya kijani kibichi,kwa kuwa mvua yenyewe huwa adimu katika kipindi cha miezi miwili inayonyesha.

Wanyama wanaofugwa eneo hilo ,wengi wao huwa mbuzi na punda au ngamia ,ambao kwa kiasi kikubwa huwa hawahitaji maji mara kwa mara kwa uwezo wao wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu,ila kwa kuwa maji ni uhai na pia huongeza afya tele kwa maisha ,wanyama hawa kwa kiasi kikubwa nyama yao huwa yenye ladha ya chini kwa kukosa maji na virutubishi vinavyotokana na maji ya mvua na mara kwa mara kwa mnyama .

Wakaazi katika eneo hili wanazidi kujiunga katika makundi ili kujaribu kuyakidhi mahitaji yao ya msingi ya kuchimba visima vya maji na kuweka kwa kuhifadhi maji ya mvua wakati kunaponyesha. Hata hivyo kuna changamoto wanazopitia katika makundi hayo wakijaribu kujiimarisha, Jane Mureithi ni Kiongozi wa chama kimoja cha Tharaka Water Sacco "Katika kipindi hiki cha miongo miwili kama meneja wa water Sacco,tumeafikia kusaidia takriban familia mia mbili hamsini ,Shule tano na hospitali tatu kwa kuwaeka katika hali shwari ya kupata maji. Hayo yote ni kwa ushirikiano na kampuni ya maji ya Kathita Water and sewerage company (KWASCO)".Licha ya hayo ametaja changamoto ya kukosa ufadhili wa kutosha kama kero kuu.

Hata hivyo wakaazi wa eneo zima la tharaka pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu hicho,wameiomba serikali ya kaunti ikishirikiana na ya kitaifa kuingilia kati swala hilo hususan katika kufadhili mpango huo wa kuwapiga jeki na vifaa vya kuchimba na kuhifadhi maji ,huku wakielekeza wito wao kwa viongozi wa eneo hilo ,kuwachimbia visima na vidimbwi vya maji ili kukabili janga hilo la ukosefu wa maji .

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow