Safaricom yashirikiana na LREB kuboresha teknolojia ya mawasiliano

May 11, 2023 - 14:50
May 11, 2023 - 15:16
 0
Safaricom yashirikiana na LREB kuboresha teknolojia ya mawasiliano
Afisa Mkuu wa Huduma za fedha katika kampuni ya Safaricom, Esther Masese. Picha/Esther Masese/Twitter.

Na Robert Mutasi

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imeshirikiana na Jumuiya ya Uchumi ya Eneo la Ziwa (LREB) ili kuongeza kasi ya mabadiliko ya kidigitali.

Akizungumza katika kikao na viongozi wa LREB nje ya mkahawa wa Kamel Kaunti ya Kisii, Mei 11,2023, Afisa Mkuu wa Huduma za fedha katika kampuni ya Safaricom, Esther Masese, amesema kuwa wanashirikiana na wahasibu na serikali za kaunti hizo ili kuwezesha uwazi wa huduma bora.

Kulingana na afisa huyu wa kampuni ya Safaricom,wanapania kuboresha teknolojia iliyothabiti na ya kuaminika itakayolinda data na mawasiliano ya serikali za kaunti.

Masese aidha amesema hatua hii itasaidia kaunti kuhudumia wananchi kwa njia rahisi ili kuendesha uchumi kwa imara na hivyo kuboresha maisha ya wakenya.

"Tutaunganisha mawasiliano na kulinda data na mawasiliano ya kaunti hizi," afisa huyo amesema.

Hata hivyo Masese amesisitiza kuwa mawasiliano imara miongoni mwa serikali itasuluhisha changamoto kadhaa na kuunganisha wananchi na serikali.

"Mawasiliano imara katika serikali yataimarisha uhusiano wa muda mrefu kwa kuunganisha umma," aliongezea afisa huyo wa Safaricom.

Safaricom vilevile imesema kuwa mradi huo utawafaidi wakazi wa maeneo hayo kwa kuwa watahusishwa ipasavyo na kutumia huduma za kidigitali.

LREB inajumuisha kaunti za Bomet, Bungoma, Busia, Homabay, Kakamega, Kericho, Kisii, Kisumu, Migori, Nandi, Nyamira, Siaya, Transnzoia na Vihiga. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow