Viongozi wa kike wahubiri amani na umoja nchini

Aug 13, 2024 - 21:00
 0
Viongozi wa kike wahubiri amani na umoja nchini
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Viongozi wa kike nchini wamehubiri amani miongoni mwa viongozi na wananchi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Wawakilishi wa Kike zaidi ya 12 kote nchini walikusanyika pamoja kwa lengo la kujadili suala la umoja.

Wakiongozwa na Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Murang’a mnamo Jumanne, Agosti 13, 2024, Betty Maina walisema kuwa taifa linaposhuhudia ghasia, wanawake na watoto ndio huathirika sana.

Walieleza kuwa migawanyiko ya kisiasa inayoshuhudiwa nchini haitawazuia wao kama akina mama kupiga hatua mbele.

"Sisi siasa hizi zingine zote za kujionesha Sisi hatuko huko. Sijui nani alisema hili na like, Sijui nani Hape I nani, Sisi hayatuhusu," alisema Betty Maina. 

Wamemsihi Rais William Ruto kuzingatia kwa undani suala la kudumisha umoja na kuonesha mfano bora kwa viongozi wengine. 

"Tulipenda William Ruto tukijua sio Mkikuyu kwa sababu akina mama wanaeka watu kwenye roho huwa hawaweki kwenye akili, kwa hivyo ukitaka tukuweke kwa akili tupende, tifundishe upendo, tufundishe kutuliza watoto wetu waache kupiga kelele wajue mama wanawashughulikia, " alisema Maina. 

Wamewasihi viongozi wanaotofautiana kisiasa kuheshimu misimamo yao au kutafuta njia sahihi ya kusuluhisha pasi na kubadilishana cheche za maneno. 

Viongozi hao waliahidi kufanya kazi pamoja ili kutekeleza sera za serikali ya Kenya Kwanza. 

Hapo awali, baadhi ya viongozi kutoka Mlima Kenya wamekuwa wakidai kuwa watawasilisha hoja bungeni ya kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani. 

Isitoshe, uhusiano baina ya Rais William Ruto na Naibu wake Gachagua umeonekana kudorora. 

Muungano wa Azimio la Umoja umeshuhudia migawanyiko huku baadhi ya vyama vikiwasilisha maombi ya kugura Muungano huo. 

Hii ni baada ya Rais Ruto kuwateua baadhi ya wanachama kutoka chama cha Orange Democratic Movement kama mawaziri katika Baraza lake la Mawiziri. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow