Waziri mteule Chirchir afichia mbinu alizotumia kupunguza gharama ya nishati
Na Robert Mutasi
Aliyekuwa Waziri wa Nishati, Umeme na Petroli Davis Chirchir amefichua jinsi Wizara hiyo ilivyofanikiwa kupunguza gharama ya kawi.
Chirchir aliteuliwa kuwa Waziri wa Usafiri na uchukuzi baada ya Baraza la Mawaziri la awali kuvunjiliwa mbali.
Akifika mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa ya kutathmini uteuzi wa Mawaziri, mnamo Ijumaa, Agosti, 2024, Chirchir ameelezea bunge utendakazi wa Wizara hiyo.
Amejitapa na kuelezea kuwa alifanikiwa kupunguza gharama ya umeme na kuwezesha kila mwananchi kumudu.
Vilevile ameelezea mbinu nyingine waliyoitumia kupunguza gharama ya kawi ni kufunga Mitambo kadhaa ya Umeme iliyoonekana kuwa ghali na kuigharimu Wizara hiyo bajeti ya pesa nyingi.
"Moja ya mambo ya maana tangu tumefanya ni kuzima Mitambo ya Umeme ambayo ni ghali sana," alisema.
Kwa mujibu wa Chirchir, mitambo hiyo ilikuwa ikigharimu takribani shilingi bilioni 10 kwa kila mwaka huku asilimia 15 ikitumika tu.
Matumizi ya nguvu za upepo ni mojawapo ya njia walizotumia kuifanya nishati kuwa nafuu kwa Wakenya.
Chirchir amefafanua kuwa nishati inayotokana na upepo gharama yake ni nafuu.
"Ili kupunguza gharama ya nishati, tulihakikisha mchanganyiko wa nishati katika uzalishaji kutoka kwa jua, upepo na jotoardhi.
"Katika mwezi wa Julai gharama zote za umeme na bidhaa za petroli ni za chini zaidi nchini katika kipindi cha miezi 15 iliyopita," Chirchir alielezea.
Kuwepo kwa mabwawa mengi ya kusambaza maji yamesaidia pakubwa katika kusitisha gharama ya nishati.
"Tumekuwa na maji mengi, hivyo tunaendesha Kiambere, Kindaruma, Kitaru, Kasikit yetu lakini kubwa zaidi yanachanganya ili kuhakikisha hatupeleki umeme wa gharama kubwa wakati hatuhitaji,” alisema.
Tayari Wizara hiyo ilikuwa imeanzisha harakati za kutumia nishati safi kwa kiwango cha asilimia 100 ifikiapo 2030.
"Changamoto ya dhamira ya mabadiliko ya tabianchi ambayo tumeiweka kwa mwaka 2030 kuwa ya kijani kwa 100%," alisema Chirchir.
What's Your Reaction?