Cate Waruguru: Mjadala wa kumbandua mamlakani Gachagua hauna maana

Jul 30, 2024 - 17:43
 0
Cate Waruguru: Mjadala wa kumbandua mamlakani Gachagua hauna maana
(Kutoka kushoto) Naibu Rais Rigathi Gachagua, Cate Waruguru na Rais William Ruto. Picha/hisani.

Na Robert Mutasi 

Aliyekuwa Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Laikipia Catherine Waruguru amedai kuwa mjadala unaendelea wa kutaka kumbandua mamlakani Naibu Rais Rigathi Gachagua hauna maana.

Amesisitiza kuwa wanaopanga njama hiyo ni watu ambao wamekuwa na kinyongo ndhidi ya Gachagua kwa mafanikio yake kama naibu wa rais. 

Kupitia pachiko lake kwenye mitandao ya Kijamii mnamo Jumanne, Julai 30, 2024 , Waruguru alisema kuwa Wakenya wanawaunga mkono Rais William Ruto na Rigathi Gachagua kinyume na madai yanayoibuliwa kuwepo kwa mgawanyiko baina ya wawili hao.

Amewakashfu wale amedai wana mipango ya kumbandua Gachagua na kuwataja kuwa wenye machungu.

"Wananchi wa Kenya wako nyuma ya Rais na naibu wake Mhe Rigathi Gachagua," taarifa ilisema.

"Hili halina mjadala, wale wanaosukuma simulizi ya kumuondoa Mamlakani ni watu wenye uchungu ambao bado hawajakubaliana na ukweli kwamba Riggy G ni Naibu Rais wa Kenya," taarifa ilisema kwa sehemu.

Waruguru amefafanua kuwa wazo la kumbandua kiongozi mamlakani limepitwa na wakati na wanaoshinikiza hatua hiyo ni wale wenye uelewa mdogo wa kisiasa. 

Amewasuta viongozi wenye njama dhidi ya Gachagua kuwa haitazaa matunda kamwe. 

Badala yake, Waruguru amewataka waelekeze nguvu zao kufanya mambo muhimu ya kujenga taifa. 

Mwanasiasa huyo ameeleza kwamba viongozi wanaojibiidisha kumuondoa Gachagua uongozini wana njama ya kuleta utengano na mgawanyiko katika serikali. 

Hata hivyo, Waruguru amewasihi viongozi kuelekeza juhudi zao kuleta umoja miongoni mwa wakenya na kuchangia ukuaji wa kiuchumi. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow