Uchambuzi: Kibarua kigumu kwa Tottenham wakiwaalika Liverpool leo
Na Robert Mutasi
Tottenham Hotspurs italazimika kukaza mkanda wake wa nishati ili kukabiliana vilivyo na Wekundu, Liverpool Leo saa moja unusu, saa za Afrika Mashariki ugani Tottenham.
Wakiwa bado wana maruerue ya mechi babu kubwa ya wikendi iliyopita waliocheza dhidi ya vijana wa Arteta, Arsenal kwenye ngarambe za EPL, mchuano uliotamatika sare ya 2-2 ugani Emirates, watavaana na Wekundu Leo.
Hakika itakuwa mechi ya patashika nguo kuchanika baina ya timu hizi mbili.
Mchuano huu unasubiriwa kwa hamu na hamumu na Mashabiki shakiki ashiki wa soka kote ulimwenguni huku kila upande ukiwa na matumaini timu yao pendwa itashinda.
Muamuzi wa mchuano wa leo atakuwa Simon Hooper ambaye atasimamia mechi kwa dakika tisini huku wababe hao wakitoana kjjasho.
Kikosi kinachokisiwa kuanza mchezo kwa upande wa wenyeji Tottenham Hotspurs ni Gugliemo Vicario, Pedro Porro, Cristiano Romero, Micky Van De ven, Destiny Udogie, Pape Matar Sarr, Yves Bissouma, Dejan Kulusevski, Richarlison, Manor Solomon na Son Heung-Min.
Liverpool huenda wakaanzisha Alison Becker, Joe Gomez, Ibrahima Konate, Virgil Van Dijk, Andy Robertson, Dominic Szoboszlai, Alexis Mac Allister, Curtis Jones, Mohamed Salah, Darwin Nunez na Luis Diaz.
Tottenham wamefunga angalau mara mbili kwa kila mechi saba za Ligi Kuu Uingereza.
Liverpool wamekuwa wakipoteza katika kipindi cha kwanza cha mchezo lakini wakashinda mwisho wa mchezo kwa nne za michuano yao ya sita.
Tottenham wanaendeleza mwanzo wao mazuri wa msimu huu chini ya ukufunzi wa kocha Anges Postecoglou na share ya 2-2 dhidi ya Arsenal wikendi iliyopita, kijasho tena kitawatoka leo.
Tangu sare ya wikendi ya ufunguzi dhidi ya Chelsea, Wekundu wameshinda mechi saba mfulululizo katika mashindano yote.
Huenda mchezo huu ukatoka sare maana kila upande umejiandaa vilivyo, Tottenham jicho likiwa kwa Sarr, Bissouma na Richarlison huku kwa upande wa Liverpool jicho likitua kwa Mo Salah's, Nunez na Diaz.
What's Your Reaction?