Watu wane watiwa mbaroni kwa shutuma za uhalifu

Turkana
Jumanne Desemba 19,2023
KNA na Peter Gitonga
Polisi mjini Lodwar leo asubuhi wametia mbaroni majambazi wanne baada ya kumpora mwanabiashara mmoja takribani Shilingi laki tatu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Kaunti ndogo ya Turkana ya kati Samuel Kiptanui,wanne hao walikamatwa mapema leo baada ya kumpora Gabriel Maraga laki tatu pesa taslimu.
Inadaiwa kuwa majambazi hao walitokea jijini Nairobi wakiwa na lengo la kufamia maduka Mjini Lodwar ila mipango yao ikafeli.
Gabriel Maraga anasema alienda Benki kutoa pesa kisha baadaye akaandamwa na majangili hao na kulivamia gari lake na kutoeka na kitita hicho.
Tukio hili limewashangaza wakazi huku wakitaka vitengo vya usalama kuwa makini msimu huu wa Krisimasi na mwaka mpya.
Wanne hao kwa Sasa wanazuiliwa katika kituo Cha polisi huku uchunguzi ukiendelea.
Hisani; KNA
What's Your Reaction?






