Wazazi walalamikia mfumo mpya wa ufadhili wa masomo

Na Robert Mutasi
Wazazi pamoja na wanafunzi wamelalamikia mfumo mpya wa ufadhili wa masomo kuwa ni ghali mno.
Wazazi wengi wamesema kuwa Karo ya shule imekuwa juu zaidi ukilinganisha na mfumo wa awali.
Kupanda kwa Karo ya shule kunawafanya wazazi wengi kutomudu kulipia watoto wao.
Wale waliofanikiwa kulipia nusu wamelalamika kwamba wanao wanakosa kufanya mitihani ya kitaifa kwa kuwa hawajamaliza Karo.
Kando na karo, malipo ya mitihani ndiyo pia yamewatatiza wengi wao.
Licha ya kuwepo na Bodi ya Ufadhili wa Elimu ya Juu (HELB) bado wanatatizika kulipia.
Wazazi hao wameitaka serikali kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu kuingilia kati suala hilo.
Rais William Ruto na maafisa kutoka Idara ya Elimu wamekuwa wakiupigia upatu mfumo huo mpya wakisema kuwa ni bora zaidi kuliko mfumo wa zamani.
Wanadai kuwa pesa ambazo zinatengewa katika mfumo mpya ni nyingi zaidi kuliko mfumo wa awali.
Wataalamu hao wa Elimu wanaeleza mfumo huu umerahisisha mbinu ya kupata fedha kwa wanafunzi ambaye ameafiki vigezo.
Mfumo huo mpya ulizinduliwa na Rais William Ruto mwezi Mei, 2023, kwa ajili ya kutatua matatizo yanayokumba vyuo vikuu na Taasisi za Kiufundi.
Mfumo huo unatazamiwa kusuluhisha tatizo la idadi kubwa ya usajili na uhaba wa ufadhili katika shule za umma.
What's Your Reaction?






