Raymond Omollo athibithisha maafisa wa polisi kupokea nyongeza ya mishahara

Aug 21, 2024 - 20:59
 0
Raymond Omollo athibithisha maafisa wa polisi kupokea nyongeza ya mishahara
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Katibu Mkuu katika Wizara ya Usalama wa Ndani na Maendeleo ya Nchi Raymond Omollo amethibisha maafisa wa polisi kupokea nyongeza ya mishahara. 

Omollo aliyasema haya baada kuidhinishwa kwa mishahara hiyo ya maafisa wa polisi katika ngazi tofauti nchini.

Nyongeza ya mishahara ilipendekezwa na ripoti ya Kikosi Kazi cha aliyekuwa Jaji Mkuu Maraga na sasa imetekelezwa. 

"Maafisa wote wa polisi wamepokea nyongeza ya mishahara kuanzia Julai 1, 2024. Katika awamu ya kwanza, maofisa waliovaa sare walipokea nyongeza ya mishahara ya asilimia 40 kwa makonstebo, huku asilimia hiyo ikipungua hatua kwa hatua kwa vyeo vya juu, hadi ongezeko la asilimia 3 kwa maafisa wakuu,” barua hiyo ilisoma katika sehemu.

Kwa mujibu wa Omollo, maafisa kutoka kitengo cha Magereza na Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYC) wataanza kupokea nyongeza ya mishahara yao kuanzia mwezi wa Septemba, 2024 jinsi alivyoelekeza Rais William Ruto.

"Kuanzia mwezi ujao, Septemba 2024, maafisa katika Huduma ya Magereza ya Kenya na Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) pia wataanza kupokea nyongeza ya mishahara kama sehemu ya agizo la Rais kuhusu utekelezaji wa haraka wa Kikosi Kazi cha Jaji Mkuu (Mst) David Maraga. mapendekezo ambayo yanatolewa katika taasisi hizi zote," taarifa ya Omollo iliyotiwa saini mnamo Agosti 21, 2024, ilisoma.

"Ili kuhakikisha utekelezaji wa mageuzi hayo unafanyika bila vikwazo, tumeanzisha Kamati za Kitaalam za Maendeleo ya Mifumo ya Sheria na Sera zinazojumuisha Huduma tatu ambazo pia zimetangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali," alisema Katibu Omollo kurejelea mipango ya kuanzia utekelezaji wa mageuzi katika idara ya polisi. 

Kulingana na Katibu Mkuu, mchakato wa mageuzi unatarajiwa kuchukua miaka minne, kuanzia 2024 hadi 2028, ukiongozwa na usimamizi na uwajibikaji, ukuzaji wa uwezo wa kitaasisi na usimamizi wa rasilimali watu, maandalizi ya uendeshaji na uwezo wa vifaa.

Mnamo Jumatatu, Juni 24, 2024, Rais William Ruto alisema kuwa Marekebisho ya mishahara ni sehemu ya ajenda pana ya mageuzi yenye lengo la kuongeza ufanisi na motisha ya jeshi la polisi.

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow