Viongozi wa kidini waibua hisia kuhusu uraibu wa teknolojia

Aug 5, 2024 - 17:42
Aug 5, 2024 - 22:04
 0
Viongozi wa kidini waibua hisia kuhusu uraibu wa teknolojia
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Viongozi wa kidini na wazazi wameibua wasiwasi wao kufuatia ukuaji wa teknolojia kwa kasi na uraibu wake kwa jamii.

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili na Asilia ya Kikristo ya Kenya(FEICCK), Askofu David Thagana, mnamo Jumatatu, Agosti 5, 2024, amesema kwamba uraibu huo umeathiri pakubwa jamii.

Askofu Thagana alifafanua kuwa athari nyingi za uraibu umeathiri ukuaji wa maendeleo kwa jamii kwani nyingi yazo ni hasi. 

"Sisi zote tumeathirika na teknolojia kwa njia moja au nyingine na jinsi tunavyoiana kwa mitazamo yetu," alisema.

"Wakati wengine Wana uraibu, sisi sote tumeathirika na teknolojia, simu, vyombo vya habari na mtandao," alisema Thagana.

Isitoshe, askofu amesema kuwa watu wengi wamepata matatizo ya kiafya kutokana na matumizi ya mara kwa mara ya teknolojia. 

Ameelezea kuwa endapo suala hili halitathibitiwa na kuangaziwa kwa undani, vizazi vya sasa na vijavyo vitaathirika zaidi. 

"Ni muhimu tujifunze ujuzi fulani juu ya njia za kudhibiti na kuamua jinsi tutakavyotumia vifaa hivi ili tusiishie kizazi cha mazombi, wapumbavu, watu ambao hawawezi kufanya uamuzi kwa sababu, walitumia muda wao kwenye simu," alisema. 

Thagana aidha amesema kuwa ni jukumu la Kila mmoja kuchukua tahadhari ya mapema na kuwa makini a teknolojia hiyo. 

"Tunawasihi wote hasa wazazi na viongozi na kaka na dada tuwe makini na aina hii mpya ya uraibu ambao ni ya kiteknolojia," alisema. 

Kwa mujibu wa Askofu Thagana, uraibu wa teknolojia utawasababishia vizazi vijavyo kutofikiria kwa kina na kufanya maamuzi yenye busara.

Alifafanua kuwa sasa hivi karibia Kila mtu ameathirika na teknolojia kwa njia moja au nyingine. 

Haya hivyo, viongozi hao walisema kuwa tayari teknolojia ameathirika jamii pakubwa, ni jukumu la kila mmoja haswa wazazi kuwa waangalifu na matumizi ya simu na teknolojia zingine kwa watoto wao. 

Kulingana na Thagana, watu wanatumia muda mwingi kwenye simu zao na ni mojawepo ya sababu zinazoleta madhara haswa kwa afya zao. 

Thagana amesisitiza kuwa uraibu huo ndio unaochangia pakubwa utendakazi katika huduma mbalimbali. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow