Mbunge wa Mathioya akanusha madai ya kumbandua Gachagua mamlakani

Aug 5, 2024 - 19:29
 0
Mbunge wa Mathioya akanusha madai ya kumbandua Gachagua mamlakani
Mbunge wa Mathioya Edwin Mugo. Picha/hisani.

Na Robert Mutasi 

Mbunge wa Mathioya Edwin Mugo amesema kuwa madai ya kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani ni uvumi.

Mugo amesema kuwa hoja hizo hazijafikishwa bungeni rasmi bali zinasambazwa chini kwa nchini na mahasimu wake. 

Haya yanajiri baada ya baadhi ya wanasiasa serikalini kuibua madai kwamba wanapanga kumuondoa mamlakani Gachagua.

Akihutubia waandishi wa Jabari, mnaml Jumatatu, Agosti 5, 2024, Mugo amesema kuwa wao kama wabunge hawajapata wasilisho lolote kuhusiana na Gachagua.

Amekanusha penyenye ambazo baadhi ya wanasiasa wanatembeza dhidi ya Gachagua na kudai kuwa wanatofautiana kisiasa.

"Kumuondoa mamlakani Gachagua kwa sasa ni uvumi, inafaa iletwe bungeni rasmi, sijaona hizi saini ambazo watu wanaongelea," alisema Edwin Mugo. 

Mugo alisema taifa lina katiba na endapo hoja ya kumbandua Gachagua italetwa bungeni, utaratibu wote wa wa kumuondoa mamlakani utafuatwa.

"Punde tu hoja itakapoletwa tutaangazia pande zote mbili, uzuri wake na ubaya wake kwenye utendakazi wake. Unajya Kenya inatawaliwa na Katiba," alisema Mugo.

Alisimulia kuwa Wakenya wengi kwa sasa Wana haja na maendeleo na huduma anayowafanyia Gachagua na wala sio suala la kumng'oa mamlakani wala siasa zake. 

" Jinsi ninavyooona, Wakenya wana haja na huduma na wala sio siasa binafsi, " alisema Mabunge Mugo. 

Kulingana na Mugo, Gachagua kwa sasa ana majukumu ya kutekeleza na kuhudumia Wakenya kama vile kumaliza pombe haramu. 

"Ana kazi ya kufanya, ana kazi ya kupigana dhidi ya pombe haramu, kuhakikisha bei ya kahawa na majani Chai zimeimarika," alieleza Mugo. 

Hata hivyo, amemsihi Gachagua kukoma kufanya kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2027 na badala yake, ayatekeleze majukumu yake. 

Mugo amesema Gachagua na viongozi engine wa kisiasa kuwa kuna haja ya kupunguza siasa kwa sasa na kutimizia Wakenya mahitaji yao. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow