Wakulima wa miwa wapinga bei mpya

Aug 19, 2024 - 19:56
Aug 20, 2024 - 16:44
 0
Wakulima wa miwa wapinga bei mpya
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Wakulima wa miwa kutoka Kaunti ya Kericho wamepinga vikali bei mpya ya miwa.

Wakulima hao walilalamikia kudhulimiwa na kutaja hatua hiyo kama njia ya kukandamiza juhudi zao.

Wakizungumza na vyombo vya habari, mnamo Jumatatu Agosti 19, 2024, wakulima hao waliitaka Mamlaka ya Kilimo na Chakula (AFA) kuingilia kati kuhakikisha wamepewa haki yao.

Bei ya miwa ya awali ilikuwa shilingi 6,100 kwa kila tani na kupunguzwa hadi shilingi 5,125 kwa tani . 

Wakulima hao waliwalaumu viongozi katika sekta hiyo kwa kulaza damu katika utendakazi wao. 

Walidai kuwa viongozi wa viwanda vya miwa wana njama ya kufaidika na pesa zinazotokana na jasho la wakulima kwa kushirikiana na watapeli. 

Walitoa onyo kali kwa usimamizi wa miwa kurejesha bei ya miwa ya awali la sivyo wataandaa mgomo wiki ijayo. 

Walieleza kuwa watakoma kupeleka miwa yao katika viwanda hadi pale watatendewe haki. 

Aidha, wakulima hao walitishia kuandaa maandamano ambayo wanasema yatachochea wafugaji na wakulima wa mazao mengine wanaohisi kudhulumiwa kugoma pia. 

Walisistiza kwamba wakulima wengi wanategemea ukulima wa miwa na hatua hiyo imewaumiza wengi.

Wakulima wengi wa miwa nchini wamekuwa wakilalamikia kucheleweshwa kwa malipo yao huku wengine wakilavilaumu viwanda vya miwa kukawia kwa muda mrefu kubeba miwa yao shambani.

Hali hii imepelekea wakulima wengine kutafuta namna ya kuuza miwa yao kwa kuwatafuta wanunuzi binafsi. 

Hatua ya serikali kuagiza sukari kutoka nchi za nje kumechangia matatizo ya wakulima wa miwa. 

Soin ni mojawepo kiwanda kilicho maarufu katika kaunti ya Kericho kile cha West Valley kikizinduliwa hivi majuzi. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow