Wahalifu kuchukuliwa hatua kali

Dec 5, 2023 - 18:09
 0
Wahalifu kuchukuliwa hatua kali
Picha: Kwa hisani.

Molo,

Jumanne Disemba 5, 2023

KNA na Emily Kadzo

Mwakilishi wa wadi ya Menengai, eneo la Nakuru Mashariki, Wilson Mwangi ametoa onyo kali Kwa watu wanaojihusisha na uhalifu wakati huu wa msimu wa Krismasi, huku akisisitiza kuwa watakabiliwa na adhabu kali za kisheria.

Mwangi alisema kuwa hawataruhusu biashara kufeli kutokana na ukosefu wa usalama.

Alisema kwamba wanapanga kuimarisha doria za polisi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Mwangi pia alionya kuwa ye yote atakayejaribu kupora mali ya wenzake au kuwadhuru wengine atakamatwa na kukabiliwa kisheria.

Aidha alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya waendeshaji bodaboda na polisi ili kuimarisha usalama na kuzuia wahalifu wa kutumia vibaya pikipiki kwa shughuli zisizo halali.

Hali kadhalika Mwangi alisisitiza haja ya ushirikiano katika kutoa taarifa zitakazosaidia polisi kuwakamata wanaovunja sheria.

Wanachama wa bodaboda katika eneo hili wamekuwa wakihangaishwa, hasa na magenge ya wahalifu kama vile 'Thibitisha'.

Katika kukabiliana na hali hiyo, kwa sasa wametekeleza utaratibu ambapo kila mwendesha bodaboda katika eneo hilo anapokea namba maalum ya kuhudumu kama hatua ya kujitambulisha.  

Hata hivyo,walipongeza juhudi za maafisa wa usalama wakisema kuwa uhalifu umepungua kwa kiwango kikubwa. 

Hisani; KNA 

 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow