Mechi ya Ufunguzi EPL: Manchester United Dhidi ya Fulham

Aug 16, 2024 - 20:02
 0
Mechi ya Ufunguzi EPL: Manchester United Dhidi ya Fulham
Picha:Hisani.

Na Robert Mutasi 

Hata kabla ya makovu ya kupoteza ushindi wa Kikombe cha Ngao ya Jamii kwa Manchester City kupoa, Manchester United watawaalika Fulham kwenye kampeni za Ligi Kuu Uingereza EPL msimu 2024/25 katika mechi ya ufunguzi. 

Manchester United inajivunia kushindakikombe cha FA wakati ikicheza na mahasimu wao kutoka jiji la Manchester, Manchester City. 

Kufuatia kichapo kutoka kwa Manchester City, kutawafanya Mashetani Wekundu kujitahidi ili kupata ushindi wa kuvutia machozi leo dhidi ya Fulham. 

Msimu uliopita Manchester United ilimaliza katika nafasi ya 8 kwenye jedwali la EPL.Msururu mbaya wa matokeo kwa timu hiyo kuwahi kutokea tangu msimu wa 1989-90.

Fulham imeandikisha sare mara mbili katika mechi zao tatu za ufunguzi za EPL. 

Manchester United imeandikisha ushindi mara nne Kati ya mechi zao 13 za mwisho EPL. 

Fulham walipandishwa daraja hadi Ligi Kuu ya EPL msimu 2021/22.Wamekuwa wakitia fora kuhakikisha wanasalia katika Ligi Kuu.

Mchuano wa leo unaonekana kuwa mkali na wa kutoana kijasho ukizingatia Manchester United wamesajili wachezaji wapya nao Fulham wanataka kutetea uwepo wao EPL. 

Katika michuano ya maandalizi ya msimu 2024-25 wachezaji wengi wa Manchester United walijeruhiwa katika mechi hizo. 

Walio na majeraha mepesi watajitahidi kucheza lakini wengine walio na majeraha makubwa wataukosa mchezo wa leo. 

Mtanange huo utachezwa katika uwanja wa Old Trafford na kuamuliwa na muamuzi raia wa Uingereza, Robert Jones. 

Kikosi cha Manchester United kinachotabiriwa Kuanza ni Andre Onana, Diogo Dalot, Matthijs de Light, Lisandro Martinez, Noussair Mazraoui, Casemiro Kobbie Mainoo, Amad Diallo, Bruno Fernandes, Alejandro Garnacho na Joshua Zirkzee. 

Huku Fulham nao wakiwa na mlinda lango Bernd Leno, Antonee Robinson, Jorge Cuenca, Issa Diop, Timothy Castagne, Sasa Lukic, Andreas Pereira, Emile Smith Rowe, Alex Iwobi, Rodrigo Muniz na Harry Wilson. 

Manchester United itakosa huduma za Luke Shaw, Victor Lindelof, Rasmus Hojlund na Tyrell Malacia ambao wanauguza majeraha. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow