Mwanamme akana Mashtaka ya kumpiga na kumjeruhi mwenzake

Jun 16, 2023 - 22:48
 0
Mwanamme akana Mashtaka ya kumpiga na kumjeruhi mwenzake
Mfungwa

Murang’a, Ijumaa, Juni 16, 2023

na Rehema Katana

Henry Mwangi Mburu alishtakiwa katika mahakama ya Murang’a kwamba mnamo Oktoba 22, 2022 katika eneo la Kambirwa, Kaunti ya Murang’a, alimpiga na kumjeruhi Francis Mbuthia Mburu.

Mishtakiwa alikana mashtaka mbele ya hakimu mkuu Eric Musambai ambapo Collins Okongo, afisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kambirwa, aliarifu kuwa mlalamishi alipigwa na mtu anayemjua. 

Mlalamishi ambaye alikua na alama ya kukatwa katika mkono wa kulia, aliandikiwa ripoti kuenda katika kituo cha afya kutibiwa na siku iliyofuata, alirudi kituo cha polisi kupeleka barua ya matibabu.

Afisa Okongo aliandika taarifa ya kesi na kuelekezwa kwa mshtakiwa, akakamatwa na kepelekwa kituo cha polisi cha Kambirwa afunguliwe mashtaka.

Mbele ya mahakama, afisa Okongo alieleza kuwa chanzo ya kujeruhiwa kwa Mbuthia ni mzozano wa familia ambao chifu wa eneo la Kambirwa ameshindwa kutataua pamoja na maafisa wa polisi.

Mlalamishi alieleza mahakama kuwa wamejaribu kutataua vita hivyo kifamilia lakini wameshindwa.

Katika utetezi wake, mlalamishi alieleza mahakama kuwa mlalamishi alikuwa na ripoti ya matibabu kabla ya kupewa barua ya P3 na afisa polisi.

Hakimu mkuu Eric Musambai aliratibisha kesi kusikilizwa tena Juni 26.

Na ; K. N. A

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow