Kenya na Mauritius yafanya mazungumzo kuhusu mageuzi ya AU

Aug 6, 2024 - 21:37
 0
Kenya na Mauritius yafanya mazungumzo kuhusu mageuzi ya AU
Rais William Ruto. Picha/hisani.

Na Robert Mutasi 

Kenya imefanya majadiliano ya nchi ya Mauritius kuhusu jinsi ya kuleta mageuzi ndani ya Umoja wa Afrika (AU).

Mazungumzo hayo yanadhamiria kuhakikisha AU inakuwa na madhumuni yanayofaa ili kupiga hatua mbele. 

Kupitia kwenye chapisho lake katika mitandao ya kijamii, mnamo Jumanne, Agosti 6, 2024, Rais William Ruto amefichua kuwa alifanya mazungungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Pravin Kumar Jugnauth.

Kiini cha mazungumzo hayo ni kutetea mageuzi katika Umoja wa Afrika.

"Kenya na Mauritius zitashirikiana kutetea mageuzi ndani ya Umoja wa Afrika ili kuhakikisha kuwa unafaa kwa madhumuni," aliandika Ruto. 

Rais Ruto pia alikuwa na nia ya kuisihi Mauritius kumpigia kura Raila Odinga katika cheo cha uenyekiti katika Tume ya AU.

Kenya inaamini aliyekuwa Waziri Mkuu Odinga ndiye chaguo bora katika cheo hicho. 

Ruto amesema kuwa Mauritius kumpigia debe Raila Odinga, itawezesha kutimiza ndoto ya mageuzi kwani Raila ana nia ya kutetea Afrika. 

"Nimekuwa na majadiliano yenye tija na Waziri Mkuu wa Mauritius Pravind Kumar Jugnauth kuhusu mageuzi ya AU na jitihada za Kenya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya AU," aliongezea Rais. 

Kwa upande mwingine Ruto ameeleza kuwa alifanya Mazungumzo ya simu na Rais wa Sudan Salva Kiir kuhusu harakati za kudumisha Amani Sudan Kusini. 

Kenya ilizindua kampeni ya Mpango wa Tumaini ili kusaidia kusuluhisha mgogoro uliopo Sudan Kusini. 

Ruto amesema kuwa makundi yote mawili yanatarajiwa kuhusishwa ili kusikilizana kuhusu taratibu za amani zilizopendekezwa. 

"Pia nilipigiwa simu na Rais Salva Kiir kuhusu maendeleo ya Amani nchi Sudan Kusini kupitia Mpango wa Tumaini. Tulisuluhisha hitaji la kushirikisha vikundi vyote na kukubaliana juu ya kutekeleza wa itifaki za Amani ambazo zimependekezwa," sehemu ya chapisho ilisoma. 

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow